Bendera ya Kristu

Bendera ya Kristu
ChoirFamilia Takatifu Katubuka Kigoma
AlbumMtu Mkamilifu
CategoryGeneral
ComposerEric Mkude

Bendera ya Kristu Lyrics

Bendera ya Kristu yapepea, na tena yaongoza jahazi
Ukiwa ndani ya Kristu ucheze
Marimba cheza hima kikristu (Bendera)
Ni bendera ya Kristu na hata Bwana,
Yatuonyesha njia ya ukweli Bwana
Yapepea inatuongoza kwa Baba mbinguni juu

 1. Bendera bendera yenye msalaba wa ushindi
  Ushindi ushindi kwa kuteswa kwake tumepona
  Bendera, bendera inatuongoza kwake Baba
  Yanipa, yanipa kila tumaini na ushindi
 2. Bendera bendera katikati yake ni msalaba
  Msalaba msalaba alama ya Kristu mshindaji
  Msalaba msalaba mti wa thamani wa bendera
  Ni mti ni mti bendera kwa huo yapepea
 3. Bendera bendera msalaba wake ni mwekundu,
  Ni damu ni damu ya Mwanakondoo mshindaji
  Kondoo kondoo aliyetolewa ni sadaka
  Sadaka sadaka kwa kuchinjwa kwake tumepona
 4. Bendera bendera pembe ni jeupe inang`ara
  Ishara ishara ya utakatifu mlovaa
  Bendera bendera haiteteleki yaongoza
  Ni njia ni njia yenye uhakika wa mbinguni

Favorite Catholic Skiza Tunes

Umerekodiwa na kwaya kadhaa * Familia Takatifu Katubuka Kigoma * Kwaya St. Austin Kanisa la St. Mary's Msongari, Nairobi ni baadhi