Chenga ya Mwili

Chenga ya Mwili
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumKidole Juu (Vol 23)
CategoryUbatizo
ComposerVictor Aloyce Murishiwa

Chenga ya Mwili Lyrics

 1. Nimempiga shetani chenga ya mwili
  Kuisalimisha roho yangu kuisalimisha roho
  Nimempokea Yesu moyoni mwangu
  Nipate uzima wa milele ili niishi milele

 2. Tazama nimebatizwa kwa nafsi tatu
  Baba mwana naye Roho Mtakatifu
  Nimempokea Kristu moyoni mwangu
  Kwa mwili na damu yake nimeshibishwa
 3. Nimempokea Roho Mtakatifu
  Amenijaza mapaji mapaji saba
  Nimeikiri imani, imani yangu
  Nimemkana shetani na mambo yake.
 4. Nikikumbuka kiapo cha ubatizo
  Najionea fahari ya ukristu wangu
  Nikikumbuka ungamo la dhambi zangu
  Ninaukiri upendo wa Yesu Kristu.
 5. Nimeshamweka kando, shetani mwovu
  Aliye mpotoshaji wa mambo mema
  Alishaniweka kwenye, imaya yake
  Alinidanganya sana na mambo yake