Ee Mungu Jina Lako Lyrics

EE MUNGU JINA LAKO

@ J. C. Shomaly

Ee Bwana Mungu jina lako ni tukufu sana
Duniani na mbinguni wewe watawala! (pia*2)
Nikiziangalia mbingu kazi ya vidole vyako
Mwezi pia na nyota Bwana umeratibisha wewe
Wanyama wa porini, ndege, samaki warukaruka!
(Njooni) njooni tumwimbie Bwana
Njooni tumwimbie Bwana, yeye ameumba vyote
Njooni tumwimbie *2 njooni tuimbe na ngoma
Piga na zeze vinanda ametuumba njooni tumwimbie}

 1. Kaumba nchi (kaumba wanyama)
  Samaki wa baharini(-rini na ndege)
  Vyote hivyo vyapendeza (-ndeza kama nini)
  Njooni imbeni (njooni tumwimbie)
 2. Mimea yote (ameumba yeye)
  Nchi yote ikajaa misitu
  Chakula chao wanyama (ni matunda yake)
  Nyama na ndege wanaruka (-ruka angani
 3. Tazama mtu (ndiye kitu gani)
  Hata wewe umkumbuke (-mbuke ee Bwana)
  Na binadamu ni nani (nani ee Bwana)
  Umwangazie (kwa wema)
Ee Mungu Jina Lako
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIR
CATEGORYZaburi
REFPs. 8
 • Comments