Enendeni Msiogope

Enendeni Msiogope
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumNakaza Mwendo (Vol 19-20)
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerFr. Mutajwaha
SourceSt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
Musical Notes
Timesignature10 16
MusickeyB Flat Major

Enendeni Msiogope Lyrics


{ Enendeni, nendeni msiogope
Lihubiri neno duniani pote, nendeni }*2


1. Enyi wanafunzi wangu mimi nawatuma
Mataifa yote nendeni mkahubiri
Nendeni kwa moyo wote wala msiogope
Shikeni vyema shauri ninalowapa ee!

2. Enjili hii viumbe vyote visikie
Ili mapenzi ya Baba yatimilike
Nyumba, anasa na mali havina nafasi
Ondokaneni na hivyo nimewatuma ee!

3. Dhiki hatari na shida havitawaweza
Giza na hila za mwovu vitayeyuka
Elewa kwamba mimi nipo nanyi daima
Ondoeni shaka kwani sitawaacha ee!

4. Nanyi mkishatimiza niliyowamuru
Posho kupata na taji mtavalishwa
Itakuwa heri gani Mbinguni kufika
Enzi nitakayopewa kuwarithisha ee!

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442