Harusi ya Kwanza

Harusi ya Kwanza
Performed by-
CategoryHarusi
Views4,016

Harusi ya Kwanza Lyrics

  1. Arusi ya kwanza ilifanywa shambani
    Mungu aliumba Adam na Hawa
    Na aliwaambia wakae wawili
    Mzae watoto mjaze dunia

    [Kuna shida kweli]
    Mtu akioa miaka mitatu tano
    matusi dharau zikaja nyumbani
    [Msipovumilia] mtaangamia
    Bwana anasema mjaze dunia

  2. Ewe bibi harusi na Bwana harusi
    Sasa mmefunga pingu za maisha
    Lakini mjue Shetani yu karibu
    Anabisha hodi kuja awatenganishe
  3. Vikwacha nyumbani nazo mtazipata
    Taabu magonjwa nyumbani mtapata
    Lakini mjue hayo ni maisha
    Yote yatokeapo mshukuruni Mungu