Haya Karibuni

Haya Karibuni
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)

Haya Karibuni Lyrics

Haya wapendwa wote mwaalika kwa karamu
Kushiriki utamu, utamu wa karamu
karamu ya Bwana *2
Amka ndugu yangu Bwana Yesu ametuita
Tukale mwili wake pia tukanywe damu yake
(twende) simama simama simama
Simama umpokee ee changamka changamka
Changamka changamka akujaze neema zake

 1. Karamu ya mapendo karamu safi na takatifu,
  Mwaalikwa wapendwa ili mpokee
 2. Wenye mioyo safi Mwokozi sasa ametuita,
  Kwa moyo safi twende wote tupokee
 3. Tutubu dhambi zetu tushiriki karamu ya Bwana
  Kwa moyo safi twende wote tupokee
 4. Ni mapendo makubwa Mwokozi yeye katulinda
  Tuleni siku zote tufike kwake