Hii ni Ekaristi Lyrics

HII NI EKARISTI

@ (traditional)

 1. Hii ni ekaristi, aliyotuachia
  Bwana Yesu Kristu (Kristu) Mkombozi wa dunia

  Imbeni - Imbeni kwa furaha
  Sifuni - Sifuni ekaristi (alimo)
  Alimo Yesu Kristu (Kristu) alimo ni mzima

 2. Yesu katuonea, wema pia huruma
  Alitupenda sana (sana) akatupa uzima
 3. Jioni Alhamisi, alichukua mkate
  Kaugeza mwili (mwili) kuleni mkaokoke
 4. Pia alichukua, kikombe cha divai
  Kakigeuza damu (damu) kunyweni kaokoke
 5. Walipokwisha kula, kawaosha miguu
  Nimewapa mfano (fano) fanyeni nanyi vile
 6. Yesu mwili na damu, chakula cha uzima
  Tujaliwe kupata (pata) uzima wa milele.
Hii ni Ekaristi
COMPOSER(traditional)
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE4
4
NOTES Open PDF
 • Comments