Inakuwaje Tunasikia

Inakuwaje Tunasikia
Performed bySt. Cecilia Ngaramtoni
CategoryRoho Mtakatifu (Pentecoste)
ComposerP. F. Mwarabu
Views18,142

Inakuwaje Tunasikia Lyrics

  1. Inakuwaje tunasikia maneno, wanayosema,
    kwa lugha yetu wenyewe
    Tunasikia mambo hayo ya Mungu, wanayosema,
    kwa lugha yetu wenyewe

    { Wao ni wa Galilaya, na si ni wa makabila,
    Ya kutoka nchi mbalimbali (duniani)
    Ina maana gani, linashangaza jambo hilo } *2

  2. Siku ile ya Pentekoste ilipofika,
    mitume nao waamini
    Walikusanyika pamoja katika nyumba,
    walimokuwa wamekaa
  3. Mara uvumi wa upepo ukasikika,
    ndimi za moto zikawashukia,
    Wakawa wamejazwa na Roho Mtakatifu,
    wakisema lugha nyingi
Also recorded by St. Paul's Students Choir University of Nairobi, volume 1.