Karibuni Watu Wote Lyrics

KARIBUNI WATU WOTE

[s] Karibuni watu wote--
[w]Twende kwake Bwana Yesu
[s] Tujongee mbele zake--
[w] Tumwabudu Mungu wetu
[t] Aai aiya--
[s] Twende wote kwa furaha tupige vigelegele
[w]Tumwimbie Mungu wetu

 1. Kama si uwezo wake hatungepata uhai
  Alleluia--atukuzwe Mungu wetu
  Kama si uwezo wake hatungekuwa na nguvu
 2. Wana wako Bwana Mungu tumekuja mbele zako
  Alleluia--atukuzwe Mungu wetu
  Twakuomba ewe Mungu upokee sala zetu
 3. Kina mama kina baba tumsifu Mungu wetu
  Alleluia--atukuzwe Mungu wetu
  Na wazee kwa vijana tumsifu Mungu wetu
Karibuni Watu Wote
CHOIR
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments