Kidole Juu

Kidole Juu
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumKidole Juu (Vol 23)
CategoryGeneral
ComposerBernard Mukasa
SourceSt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
Musical Notes
Time Signature6
16
Music KeyE Major
NotesOpen PDF

Kidole Juu Lyrics

  //utangulizi//
   Hayo mliyofunuliwa, bila kuyalipia kitu,
   Nayo ndiyo yale mliyotumwa,
   Kwenda kwa walio wadogo
   Mungu alowatunukia awe mkuu peke yake
   (Jiulize) nani kwenu (aliyeomba) kuzaliwa!
   (Jiulize tena) nani kwenu (anayejua) siku ya kufa!
   Hakuna! Hakuna! ha!

Hakuna jambo mnalomiliki hapa duniani
Yote mliyo nayo yana mwenyewe mnamjua
Naye amewapa haya kusudi mtumikiane
Ili kusiwepo na matabaka miongoni mwenu
Hiyo ndiyo hekima - ee aa ee
Hiyo ndiyo hekima -
Ndugu hiyo ndiyo hekima ya kweli } *2

 1. Kama mliyo nayo yote yangekuwa yenu
  Hiyo pumzi mnayojivunia wapendwa,
  Isingekuwa inakiogopa kichomi
  Ingeendele-a hata palipo kichomi!
 2. Uzuri wa sura zenu zenye ngozi laini
  Inakuwaje hamuwezi kuuelekeza,
  Usiungue hata kwenye maji ya moto
  Na usioze unapolala kaburini!
 3. Elimu na vyeo vyenu na mamlaka yenu
  Akili nyingi ufundi navyo vipaji vyenu,
  Mbona hamvitumii nyi mkiwa usingizini
  Na mnaota ndoto sawa na za watoto!
   //hitimisho//

   Basi mimi, ninahimizwa, kujiepusha, kujiinua
   Nijishushe, mbele ya wote,
   Wawe wakubwa, au wadogo
   Nisijiinue kati ya watu hata siku moja,
   Badala yake nijinyenyekeze ili nifikike,

   Akihitajika atakayewatumikia watu
   Niinue kidole juu kusudi wanitume mimi, daima
   Kidole juu kusudi wanitume mimi
   Kidole juu, kuitikia wito daima
   Kidole juu, kusudi wanitume mimi
   Na nikitumwa niwe mwaminifu daima
   Kidole juu, kusudi wanitume mimi
   Kidole juu wanitume na Mungu atukuzwe daima
   Kidole juu, kusudi wanitume mimi

   Kidole juu, kidole juu, leo
   Kidole juu, kusudi wanitume mimi
   Kidole juu, kidole juu, daima
   Kidole juu, kusudi wanitumie mimi, milele!

Favorite Catholic Skiza Tunes

Second version of this song is Nitumwe Mimi, that replaces the words 'Kidole Juu kusudi wanitume mimi' with 'nijitokeze kusudi wanitume mimi' And alters the title to 'Nitumwe Mimi'
* Also See Nitumwe Mimi