Kilio cha Mjane

Kilio cha Mjane
ChoirSt. Cecilia Mirerani
AlbumMchanganyo
CategoryFamilia
ComposerE. A. Minja

Kilio cha Mjane Lyrics

 • Ni nani wa kuwasaidia na kuwajali wajane
  Ni sisi tuliowapenda walipokuwa na waume zao
  Ni nani wa kuwasaidia na kuwajali wajane
  Ni sisi tuliowapenda na sasa tunawadhulumu hao

 • {Tazama leo ni sisi wenyewe chanzo cha huzuni kwao
  Tazama leo ni sisi wenyewe chanzo cha machozi yao } *2
  { Ni nani atakayekisikiliza kilio cha mjane
  Ni nani atakayekijali kilio cha mjane } *2
 • Mlishirikiana nao vizuri walipoifunga ndoa yao
  Tazama bibi harusi walimkaribisha kwa nderemo
  Nderemo nderemo tushangilie kaka yetu leo kapata jiko
  Karibu karibu wifi karibu karibu hapa ni kwako
 • Maisha mazuri maisha magumu ilikuwa ni siri ya wawili
  Maisha kufanikiwa hiyo ni siri ya baba na mama
  Maisha ya ndoa yakitenguka baba mwenye nyumba akitutoka
  Hatamu tunaishika kuchukua mali za marehemu
  Wewe utachukua gari lile, mashamba yake mimi nitayatunza
  Na nyumba ya marehemu ataisimamia kaka yetu
  Mama na watoto tunafukuzwa thamani ya utu wetu haipo
 • Wengine wanachukua watoto wa marehemu wakawasomeshe
  Na kumbe ni hila tupu wanafanyizwa kazi ngumu ngumu
  Kupika na kudeki kazi yao kufua nguo hata na kupasi
  Huruma itakujia ukiwaona wanavyotetesha
  Ndugu yangu leo ninakuomba mimi nawe sasa tubadilike
  Na tuwe kitu kimoja mfano wa kuigwa na jamii
  Tuonyeshe na kudhamini haki za wajane hata na kuwajali
  Watoto tuwajengee misingi bora ya baadaye