Kimya ni Cha Nini

Kimya ni Cha Nini
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)

Kimya ni Cha Nini Lyrics

Kimya kimya ni cha nini Bwana Yesu ametualika
Kushiriki karamu yake, karamu ya mapendo
Siku ile iliyotangulia kifo chake
(Aliwaita wanafunzi wake) *2 akawaambia

 1. Huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu
  Kuleni huu ili mpate uzima wa milele,
  (Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeni
  kushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2
 2. Hii ndiyo damu yangu itakayotolewa kwa ajili yenu
  Kunyweni hii ili mpate uzima wa milele
  (Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeni
  kushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2
 3. Amini ninawaambieni alaye mwili na kunywa damu
  Bila kustahili atahukumiwa siku ya mwisho,
  Lakini alaye mwili na kunywa damu kwa kustahili
  Nitamfufua siku ya mwisho
  (Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeni
  kushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2