Lo Bwana! Mbona Unameza Mate?

Lo Bwana! Mbona Unameza Mate?
Performed by-
CategoryHarusi
Views3,405

Lo Bwana! Mbona Unameza Mate? Lyrics

  1. Lo Bwana mbona unameza mate na hakuna chakula
    Kwani wewe huna macho huoni ile keki
    Iiliyo pale mbele kumbe tutashiba

    Enyi maarusi kateni keki tuanzeni kula
    Kwani watu wameanza kunyongwana mate

    Lakini kateni keki kwa utaratibu
    Isije ikaanguka nasi tukakosa kula
    Kwani watu wasipoonja keki hiyo
    Hawatatambua kwamba hii ilikuwa ni arusi

  2. Mwenzangu haraka sasa ya nini mbona wanikanyaga
    Kama keki hutapata mahali we ulipo
    Kwa hivyo jitulize, wacha kunifinya
  3. Kumbuka enyi maharusi keki hii ina maana kubwa
    Kwani keki ni ishara ya kuwaunganisha
    Muwe kitu kimoja msaidiane