Maisha Yangu

Maisha Yangu
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumMSHIPI (VOL. 22)
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerG. Tesha
Views17,504

Maisha Yangu Lyrics

  1. Maisha yangu
    Maisha yangu ni Yesu Kristu (Bwana wangu)
    Uhai wangu
    Uhai wangu ni Yesu Kristu (Mwokozi) } * 2

    { (Haya)
    /s/ Enyi wapenzi wa Bwana njoni mjiunge nami, tumsifu Bwana Mungu wetu
    /a/ Enyi wapenzi wa Bwana wangu njoni pamoja nami, tumsifu Bwana Mungu wetu
    /t/ Enyi wapenzi wa Bwana wangu njoni mjiunge nami tumsifu Bwana Mungu wetu
    /b/ Enyi wapenzi wa Bwana tumwimbie Bwana pamoja nami,
    Tumsifu Bwana Mungu wetu } *2

  2. Anajua kula yangu, anajua vaa yangu
    Anajua niendapo, anajua nitendalo
    Maisha yangu yamo mikononi mwake
  3. Anajua mwanzo wangu anajua mwisho wangu
    Anajua nilalapo, anajua niamkapo
    Tegemeo la maisha yangu ni Yesu
  4. Ananipa kila kitu, ananipa na uhai
    Yeye anikumbatia kama mwana wake mpenzi
    Pumzi zangu zatoka kwake Bwana wangu
  5. Upendo wake ajabu, huruma yake amini
    Msamaha wake kwangu, daima ni wa milele
    Ama kweli maisha yangu ni kwa Yesu