Mama Pale Msalabani

Mama Pale Msalabani
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Mama Pale Msalabani Lyrics

Mama pale msalabani, macho yatoka machozi
Akimwona mwanaye, kweli ni huzuni kubwa

 1. Kweli vile akilia, uchungu kama upanga,
  Ukampenya moyowe
 2. Mwenye moyo mgumu nani, asimhurumie basi
  Mama amlilia mwana
 3. Ewe Mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
  Moyo wangu mwenye dhambi
 4. Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie
  Pamoja na ukombozi
 5. Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi
  Wa uchungu na msiba
 6. Nisianguke motoni, uniwie msimamizi,
  Ewe bikira mwema
 7. Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho
  Ewe Mwokozi wangu
 8. Nitakapokufa mimi, upokee roho basi
  Niende kwako Mungu

  Mama Pale Msalabani (alternative)

 1. Mama pale msalabani, macho yatoka machozi
  Akimwona mwanaye, akimwona mwanaye
 2. Kweli vile akilia, uchungu kama upanga,
  Ukampenya moyowe, ukampenya moyowe
 3. Mwenye moyo mgumu, nani asimhurumie basi
  Mama mlilia mwana, mama mlilia mwana?
 4. Ewe mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
  Moyo wangu mwenye dhambi, moyo wangu mwenye dhambi
 5. Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie
  Pamoja na ukombozi, pamoja na ukombozi
 6. Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi
  Wa uchungu na msiba, wa uchungu na msiba
 7. Nisianguke motoni, uniwie msimamizi,
  Ewe Bikira mwema, ewe bikira mwema
 8. Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho
  Ewe Mwokozi wangu, ewe Mwokozi wangu
 9. Nitakapokufa mimi, upokee roho basi
  Niende kwako Mungu, niende kwako Mungu