Mbegu Nyingine

Mbegu Nyingine
ChoirSt. Benedict Rapogi
AlbumMbegu Nyingine (Vol 2)
CategoryZaburi
ComposerOchieng Odongo
ReferencePs. 65

Mbegu Nyingine Lyrics

{ [s] Mbegu nyingine zikaanguka
[w] Mbegu nyingine (zikaanguka)
Mbegu nyingine zikaanguka penye udongo mzuri! } *2
Zikamea, zikamea na tena zikazaa *2

1. Umeijalia nchi na kuistawisha,
Mto wako Bwana umejaa maji mazuri

2. Wewe unawaruzuku watu wote nafaka,
Na umeuvika mwaka taji ya wema wako

3. Pia na matuta yake maji umeyajaza,
Wapasawazisha popote palipoinuka

4. Wailainisha nchi kwa manyunyu ee Bwana,
Hata na mimea yake wewe waibariki

5. Kila upitapo kweli pamejaa unono,
Huyadondokeza na malisho yote nyikani

6. Na vilima vyote vajifunga nayo furaha,
Na malisho yote yamevikwa nao kondoo

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Huniongoza Mwokozi 5814856
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Tazama Tazama 7482442