Login | Register

Sauti za Kuimba

Mbinguni Kutakuwa Raha Lyrics

MBINGUNI KUTAKUWA RAHA

@ J. C. Shomaly

Nakiri kuwasimulieni na kuwapa siri hii hakika
Mbinguni kutakuwa raha kwa wale wote watakaofika
Hili jambo labidi nitamke kwani nimefikiria hakika
Hakutakuwa rushwa hongo, hirizi wala mlango wa kona,

Heri waliochaguliwa kufurahi na Mwanakondoo
Waliovumilia shida, starehe na anasa za nchi

Ole wenu (ole), ole wenu (ole) ole wenu mnaocheka sasa
Mtalia (nyinyi) mtalia (nyinyi) mtalia na kuomboleza
Ole wenu (ole) Ole wenu (ole) ole wenu mpiganao sasa
Fainali yake inakuja mshahara ni mauti

 1. Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao rushwa
  Siku zinakuja nayo rushwa pia itakuhukumu
 2. Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao wizi
  Siku zinakuja vyote ulivyoiba utarudisha
 3. Furahini furahini nyinyi mpendao haki
  Siku zinakuja mtakuwa wakuu wa wafalme
 4. Furahini furahini mtesekao kwa dhiki
  Siku zinakuja ufalme wote utakuwa ni wenu
Mbinguni Kutakuwa Raha
ALT TITLEOle Wenu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
8
 • Comments