Mfanyieni Shangwe Lyrics

MFANYIENI SHANGWE

Mfanyieni Shangwe (shangwe) dunia yote
Na mtumikieni kwa furaha (nyote) *2

 1. Njoni mbele zake, zake kwa kuimba
  Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu *2
 2. Ndiye alituumba tu watu wake,
  Watu wake na kondoo wa malisho yake *2
 3. Ingieni malangoni kwa kukushukuru
  Nyuani mwake kwa kusifu
 4. Mshukuruni lihimidini jina lake
  Kwa kuwa Bwana ndiye mwema *2
 5. Na rehema zake ni za milele
  Uaminifu wake vizazi na vizazi *2
Mfanyieni Shangwe
CHOIROur Lady of Fatima Kongowea
ALBUMKila Mwenye Pumzi (vol 4)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
REFPs. 100
 • Comments