Login | Register

Sauti za Kuimba

Mke Mwema Lyrics

MKE MWEMA

Mke mwema, mke ni nani, awezaye kumuona
Kima chake, kima chapita, kima cha marijani
{Moyo wa mumewe unamwamini,
Wala hatakosa kupata mapato *2}

 1. Humtendea mema wala si mabaya,
  Siku zote zote za maisha yake
 2. Hutafuta sufu sufu na kitani,
  Taa yake haizimiki usiku
 3. Huwakunjulia maskini mikono,
  Huwanyooshea wahitaji mikono
 4. Mwanamke yule amchaye Bwana,
  Na huyo ndiye atakayesifiwa
 5. Mpe mapato ya mikono yake,
  Basi na kazi yake yamsifu

  ~ (Prov 31)
Mke Mwema
CHOIR
CATEGORYHarusi
 • Comments