Login | Register

Sauti za Kuimba

Mpende Adui Lyrics

MPENDE ADUI

@ M. Z. Yohana

 1. Bwana Yesu alituachia amri ya mapendo
  Ili tupendane kama yeye alivyotupenda
  Tena akasema, akasisitiza,
  Mpende jirani, kama nafsi yako

  { Mpende - adui yako
  Mpende - muombee neema
  Mpende - adui yako
  Mpende - muombee Baraka } *2

 2. Sisi tulivyoumbwa wanadamu hatulingani
  Kwa tabia kwa maisha hata kwa matendo yetu
  Wapo wa hekima, wasemao ukweli,
  Na wenye kiburi, wasio na busara
 3. Hata ukinyanyaswa jitahidi kuvumilia
  Usiwe mwenye ghadhabu ukalipiza kisasi
  Ukihuzunishwa, mkimbilie Yesu,
  Atakupa faraja, heri na fanaka
 4. Usikumbuke ubaya uliokwisha tendewa,
  Hiyo itakuwa njia ya kukaribisha chuki
  Ukisha samehe, usahau yote,
  Ukatae yote, yasiyo ya hekima
Mpende Adui
ALT TITLEAmri ya Mapendo
COMPOSERM. Z. Yohana
CHOIRSt. Cecilia Kajiado
ALBUMImani Kipimo
CATEGORYLove
 • Comments