Mpigieni Bwana

Mpigieni Bwana
Performed by-
CategoryZaburi
Views5,583

Mpigieni Bwana Lyrics

  1. Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wacha Mungu,
    Kusifu kwawapasa *2 (wenye) wenye moyo mnyofu

  2. Enyi watumishi wa Bwana lisifuni,
    lisifuni jina la Bwana
  3. Jina la Bwana litukuzwe,
    Sasa na hata milele
  4. Toka mawio ya jua na hata machweo yake
    Jina la Bwana lisifiwe
  5. Bwana ametukuka juu ya mataifa yote
    Utukufu wake wazipita mbingu
  6. Nani ni sawa na Bwana,
    Mungu wetu aketiye juu?
  7. Humwinua fukara kutoka mavumbini
    Na kumkweza maskini kutoka unyonge