Ee Mungu Uniokoe Lyrics

EE MUNGU UNIOKOE

@ Charles Ruta

[b] Ee Mungu uniokoe
[w] Maana maji yamepita mpaka nafsini mwangu
[b] Ee Mungu uniokoe
[w] Ninazama katika matope mengi
{[a] Pasipowezekana (Bass) Kusimama
[w] Nimefika penye maji ya vilindi
Mtondo wa maji unanigharikisha *2}

 1. Nimechoka kwa kulia kwangu koo yangu imekauka
  Macho yangu yamedhoofu
  kwa kumngoja Mungu wangu
 2. Wanaoonichukia bure ni wengi
  `Kuliko nywele za kichwa changu
 3. Ee Mungu waujua upumbafu wangu
  Wala hukufichwa dhambi yangu
Ee Mungu Uniokoe
COMPOSERCharles Ruta
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMungu Yule
CATEGORYZaburi
REFPs. 69
 • Comments