Mwimbieni Bwana Lyrics

MWIMBIENI BWANA

Mwimbieni Bwana, mataifa ya dunia
Mwimbieni Bwana litukuzeni jina lake

 1. Tangazeni wokovu wake siku kwa siku
  Yaelezeni mataifa utukufu wake
 2. Utukufu na uzuri unamtangulia, Enzi na
  wangavu zimo katika kikao chake kitakatifu
 3. Mpeni Bwana enyi jamii za mataifa
  Mpeni Bwana sifa na enzi
 4. Mpeni Bwana utukufu wa jina lake
  Toeni sadaka ingieni katika sebule zake
 5. Semeni kati ya mataifa, Bwana ni mfalme
 6. Atatawala ulimwengu kwa haki
  Na mataifa kwa uaminifu wake
 7. Atukuzwe Baba na mwana, na Roho Mtakatifu
  kama mwanzo na sasa, na siku zote milele.
  Amina.
Mwimbieni Bwana
CHOIR
CATEGORYEntrance / Mwanzo
REFPs. 96
 • Comments