Nainua Moyo Wangu Lyrics

NAINUA MOYO WANGU

@ (traditional)

 1. Nainua moyo wangu kwako wewe ee Baba,
  Unikinge na uovu, tumaini wewe tu
 2. Nijulishe njia zako nifundishe ukweli
  Hekimayo niongoze, tumaini wewe tu
 3. Ee Baba ukumbuke wema wako milele,
  Nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu
 4. Nitazame kwa huruma ewe Mungu amini,
  Nitubishe mwenye dhambi, tumaini wewe tu
 5. Shida zangu angalia, niokoe dhikini
  Nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu
 6. Njia zako zote Bwana nifadhili na kweli
  Niongoze mtoto wako, tumaini wewe tu
Nainua Moyo Wangu
COMPOSER(traditional)
CHOIRSt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CATEGORYGeneral
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE4
4
 • Comments