Natamani Kwenda Mbinguni Lyrics

NATAMANI KWENDA MBINGUNI

@ Alfred Ossonga

Watakatifu wa Mbinguni
waimba nyimbo za shangwe
Na malaika wake Mungu
wanarukaruka kwa shangwe
Natamani kwenda mbinguni,
nikaimbe nyimbo za shangwe
Nijiunge na malaika,
nikaruke mbele za Mungu

 1. Ewe mpenzi wa moyo, ewe mlinzi wa roho,
  Roho yangu mimi,
  Nakusihi sana ewe somo wangu, nishike mkono
  Niongoze vyema nikajiunge nawe
 2. Ee malaika wa Mungu, shuka kutoka Mbinguni,
  Njoo kwangu mimi
  Nakusihi sana nipe mbawa zako, na mimi niruke
  Nifike mbinguni nikajiunge nanyi
 3. Nyinyi mlioyashinda majaribu yake Mungu,
  Hapa duniani
  Twawasihi sana mkatuombee, na sisi tushinde
  Majaribu haya tukajiunge nanyi
 4. Matendo yaliyo mema, maneno yale mazuri,
  Moyo wa mapendo
  Zitaniongoza siku zangu zote, za maisha yangu
  Hadi nije huko nikajiunge nanyi
Natamani Kwenda Mbinguni
ALT TITLEWatakatifu wa Mbinguni
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYTafakari
 • Comments