Login | Register

Sauti za Kuimba

Nawapa Amri Lyrics

NAWAPA AMRI

Nawapa amri - amri pendaneni (asema Bwana )
{ Kama vile mimi nilivyowapenda nyinyi
(Nanyi) Nanyi pia mpendaneni } *2

 1. Wapenzi na tupendane, neno latoka kwa Mungu
  Na pia apendaye amezaliwa na Mungu,
  (Naye) Naye anamjua Mungu, tupendane
 2. Yule asiye na pendo, hakumjua Mungu wetu
  Kwa maana Mungu ni mwenye upendo kamili
  (Naye) Naye ametuamuru, tupendane
 3. Mungu apenda dunia kwa mapendo yake kwetu
  Akamtuma mwanaye mwana wake wa pekee
  (Hapa) Hapa kwetu duniani, tupendane
 4. Kila amkiriye Yesu, kuwa ni mwana wa Mungu
  Ndipo Mungu anakaa, ndani yake mtu yule
  (Naye) Naye ndani yake Mungu, tupendane
Nawapa Amri
CATEGORYLove
REFJn 15:9-17 ; 1 John 5:7-21
 • Comments