Ni Nani Kama Mungu

Ni Nani Kama Mungu
ChoirSt. Cecilia Zimmerman
CategoryGeneral

Ni Nani Kama Mungu Lyrics

Ni nani awezaye kufananishwa na Mungu
Ni kitu gani kiwezacho kufananishwa na Muumba*2
Wiki nzima amenipa nguvu amenipa na uhai
Nimefanya kazi zangu zote kwa ratiba zangu zote
Na sasa niko hapa mbele kuutangaza wema wake
Waumini simameni—pigeni vigelegele
Na tuimbe pamoja tutangaze wema wake

 1. Hebu fikiria ndugu ilivyo maajabu wewe
  Umempa nini Bwana wetu muumba
  Ni wengi waliopenda kuiona siku hii
  Kwa mapenzi yake yeye wote wote hawakuiona
 2. Hebu fikiria pia ilivyo maajabu wewe
  Una maisha bora pia ya kupendeza
  Ni wengi hawana nyumba hawana na makazi
  Viungo vya mwili mikono na hata miguu

Favorite Catholic Skiza Tunes