Nimeingia Kwako

Nimeingia Kwako
Performed by-
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerF. A. Nyundo
Views14,958

Nimeingia Kwako Lyrics

  1. Nimeingia (kwako) hapa mahali patakatifu
    Unipokee (Bwana) unitakase nipate neema

  2. Nimeingia kwako nimeingia
    Hapa mahali patakatifu
  3. Ee Bwana mwema wewe mfadhili sana
    Nakuja kwako kukutukuza
  4. Nakuabudu pia nakusujudu
    Nisaidie mimi ni wako
  5. Mimi mkristu pokea sala zangu
    Ninakuomba msaada wako
  6. Nihurumie kwani mimi mnyonge
    Nategemea msaada wako
  7. Unipokee kwako unipokee
    Unitakase nipate neema