Nimekukimbilia Wewe

Nimekukimbilia Wewe
ChoirTBA
CategoryGeneral

Nimekukimbilia Wewe Lyrics

Nimekukimbilia wewe wewe Bwana wangu
Nisiaibike milele nisiaibike milele
Milele milele nisiaibike nisiaibike milele

 1. Nimekukimbilia wewe nimekukimbilia wewe
  Bwana nisiaibike milele, kwa haki yako uniponye
  Unitegee sikio lako uniokoe hima
 2. Uwe wangu mwamba wa nguvu,
  Nyumba yenye maboma ya kuniokoa,
  Ndiwe genge langu na ngome yangu
  Kwa ajili ya jina lako uniongoze unichunge
 3. Umwangaze mtumishi wako kwa nuru yako
  Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako,
  We ni hodari mpige moyo konde
  Ninyi nyote mnaongoja mnaomngoja

Favorite Catholic Skiza Tunes