Login | Register

Sauti za Kuimba

Nimeonja Pendo Lako Lyrics

NIMEONJA PENDO LAKO

@ Bernard Mukasa

 1. Nimeonja pendo lako, nimejua u mwema
  Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe
  Nitawaongoza vyema waimbe kwa furaha
  Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe.

  Ukarimu wako Bwana, na huruma yako wewe
  Msamaha wako Bwana, na upole wako (wewe)
  Umenitendea wema usiopimika
  Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

 2. Kina mama simameni, piga vigelegele
  Na kina baba nyanyuka mkapige makofi
 3. Watu wote nesanesa chezeni kwa furaha
  Inua mikono juu, mshangilieni Bwana
 4. Watawa washangilie, makasisi waimbe
  Walei warukeruke, waseme aleluya
 5. Vitambaa mikononi, vipeperushwe juu
  Na vichwa viyumbeyumbe kwa mwendo wa kuringa -
 6. Nitakushukuru mimi, na nyumba yangu yote -
  Nitayatangaza haya, maisha yangu yote -
Nimeonja Pendo Lako
ALT TITLENitawainua Wote
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMNikiziangalia Mbingu (vol 18)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
8
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
NOTES Open PDF
 • Comments