Nitamhimidi Bwana

Nitamhimidi Bwana
ChoirSt. Charles Lwanga Kisii
CategoryEkaristia (Eucharist)
ReferencePs. 34

Nitamhimidi Bwana Lyrics

Nitamhimidi Bwana kila wakati
Sifa zake zi kinywani mwangu daima
Nafsi yangu itajisifu kwake Bwana
Wanyenyekevu wasikie wafurahi

 1. Macho ya Bwana hutazama wenye haki
  Masikio yake husikia kilio
  Uso wake ni juu ya watenda mabaya
  Onjeni muone kuwa Bwana yu mwema
 2. Walilia naye Bwana akasikia
  Akawaponya na akawafuta machozi
  Yu karibu kwa waliovunjika moyo
  Onjeni muone kuwa Bwana yu mwema
 3. Mateso ya mwenye haki kweli ni mengi
  Lakini Bwana humponya nayo yote
  Huhifadhi mifupa yao yote
  Onjeni muone kuwa Bwana yu mwema