Login | Register

Sauti za Kuimba

Nitayasimulia Matendo Lyrics

NITAYASIMULIA MATENDO

@ J. C. Shomaly

 1. Nitayasimulia matendo yako Bwana
  Mungu wangu unayenipa nafasi tele
  Unayejua kuishi kwangu siku zote
  Mungu wangu unayenipa nafasi tele

  Ulinijua Bwana tangu ningali tumboni
  Maisha yangu umepanga yangali vema
  Mimi niutazame uso wako katika haki
  (Na sasa) Niamkapo nishibishwe!
  Nishibishwe! Nishibishwe (eeeh)
  Niamkapo nishibishwe
  Nishibishwe kwa sura yako

 2. Umenipa uhai na hewa ya kutosha -
  Mvua pia jua za kunilisha mimi -
 3. Elimu maarifa yasiyo na kifani -
  Niko na miguu nimejua kufanya kazi -
 4. Kazi zangu zote umenipa wewe Bwana -
  Ninajua wengi siyo kama mimi Bwana -
 5. Kwa hayo yote sina budi kukushukusu -
  Wabariki yatima pia mama wajane -
Nitayasimulia Matendo
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Cecilia Zimmerman
ALBUMNitasimulia Matendo (Vol 6)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments