Njooni Tumwimbie

Njooni Tumwimbie
Performed byOur Lady(Star of the Sea) Kenya Navy
AlbumTumeandamana
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerAlfred Ossonga
Views9,559

Njooni Tumwimbie Lyrics

  1. Njooni tumwimbie Bwana wetu - kwa shangwe
    Njooni kwa masifu kwa nderemo - tucheze
    {Njooni tuabudu, njooni tusujudu
    Tupige makofi,
    Mbele zake Bwana, Mungu wa ulimwengu } *2

  2. Hekalu lake Bwana Mungu linapendeza,
    Nyumbani mwake Bwana mna mengi mazuri
    Ninatamani kuingia nyumbani mwake
    Nikae naye siku zote nyuani mwake
    Nipate heri, mbele za Bwana
  3. Mapema leo ninabisha lango ee Bwana
    Nifungulie nipokee nipe faraja
    Nimelemewa na mizigo mingi ya dhambi
    Nyumbani mwake Bwana ndiko kuna uzima
    Uzima tele, na usalama
  4. Twendeni sote kwake Bwana Mungu Mwenyezi
    Twendeni kwake tupeleke maombi yetu
    Tutoe shukrani zetu kwa Mungu Baba
    Tutoe na dhabihu zetu kwake Muumba
    Sadaka zetu, azipokee
  5. Uhai wetu unatoka kwake Muumba
    Tuimbe sifa zake Mungu siku kwa siku
    Tuyatangaze maajabu yake popote
    Tuseme Bwana ametenda mambo makuu
    Kwa watu wote, milele yote.