Nota Mpaka Mbinguni Lyrics

NOTA MPAKA MBINGUNI

@ Jerome M.

 1. Tumetafiti tukauliza, maandiko tukafunua
  Kutambua watakatifu, wanafanya kazi gani Mbinguni

  |s1| Usiku na mchana, jioni na asubuhi
  Kiangazi masika mpaka Mbinguni

  |s2| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia
  Watunzi tutampangia nota mpaka mbinguni

  |a| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia
  Watunzi Tutampangia nota mpaka Mbinguni

   |t| Tutamsifu, waimbaji tutamwimbia, watunzi
  tutampangia nota mpaka Mbinguni (waumini)

  |b| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia
  Watunzi tutampangia nota mpaka Mbinguni

 2. Enyi wasomi tuambieni, wanasayansi tujibuni
  Katika mambo ya mbinguni, nini kinafanyika duniani
 3. Tumetambua kule mbinguni, hakuna kwenda ofisini
  Wala kumbi za burudani, hata kilimo hakuna lakini
 4. Kumbe furaha za dunia hii, ni upumbafu ni wazimu
  Na anasa za maadili, sisi waimbaji tumeamua
 5. Waamini wote furahini, makasisi shangilieni
  Nanyi watawa jiungeni, kwa waimbaji hakuna matata
 6. Upendo wake ni wa ajabu, fadhili zake za milele
  Huruma yake ni amini, msamaha wake unashangaza
Nota Mpaka Mbinguni
COMPOSERJerome M.
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMchanganyo
CATEGORYUtume wa Uimbaji


, Mbinguni


 • Comments