Nyanyukeni Wote

Nyanyukeni Wote
ChoirSt. Anthoney Malindi
AlbumMalindi Kuna Nini
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerAlfred Ossonga

Nyanyukeni Wote Lyrics

 1. Njooni tucheze mbele zake Bwana, wa mapendo
  Njooni tutoe shukrani zetu -siku zote

  Kwa shangwe
  { Nyanyukeni wote - tuimbe tumtukuze Bwana
  Tuyasimulie - pamoja matendo yake makuu } *2
  Mwilio tumekula - asante tunashukuru
  Damuyo tumekunywa - asante tunashukuru,
  Asante, kwa ukarimu, asante, kwa wema wako,
  Asante, Kwa kutulisha, asante,
  kwa kutunywesha, asante sana

 2. Njooni wazee hata na vijana - na watoto
  Njooni wamama nanyi wasichana - tufurahi
 3. Njooni tutoe ushuhuda wetu - hadharani
  Njooni tuyatangaze maajabu - yake Bwana
 4. Njooni katika madhabahu yake - takatifu
  Njooni katika sinagogi lake - tumsifu
 5. Njooni tupate baraka za Bwana - Mungu wetu
  Njooni tuishi naye tangu leo - na milele