Posho Langu

Posho Langu
ChoirSt. Anthoney Malindi
AlbumMalindi Kuna Nini
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerAlfred Ossonga
ReferencePs. 16

Posho Langu Lyrics

Bwana ndiye fungu la posho langu,
Na la kikombe changu
{Wewe unaishika kula yangu,
Nimemwambia Bwana, Bwana
Wewe ndiwe Bwana wangu } *2

 1. Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri
  Na mtima wangu, umenifundisha usiku
  Nimemweka Bwana mbele yangu daima
  Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu sitaondoshwa
 2. Kwa hivyo moyo wangu, unafurahi moyo wangu
  Washangilia, nao mwili wangu utakaa
  Kwa kutumaini, Maana wewe Bwana
  Hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu
 3. Utanijulisha njia, njia ya uzima
  Mbele ya uso wako, ziko furaha tele,
  Na katika mkono wako wa kuume
  Mkono wa kuume mna neema ya milele
 4. Mungu nihifadhi mimi, maana nakukimbilia
  Wewe Mungu wangu, Bwana ndiwe Bwana wangu,
  Wewe Bwana ndiwe fungu la posho langu
  Na la kikombe changu wewe unaishika kula yangu