Roho Ndiyo Itiayo Uzima Lyrics

ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA

@ J. C. Shomaly

{ Roho ndiyo hiyo itiayo uzima
(Mwili) Mwili haufai kitu haufai kitu
Maneno hayo niliyowaambia ni roho,
Tena ni uzima } *2

 1. Sheria ya Bwana ni kamilifu,
  Huiburidisha nafsi yangu
  Maagizo yake ni ya adili huufurahisha moyo wangu
 2. Kicho chake Bwana ni kitakatifu,
  Kinadumu milele na milele
  Hukumu za Bwana nazo ni kweli,
  Zina haki kabisa kabisa
 3. Tena mtumishi wako huonywa,
  Katika kuzishika dhawabu
  Kuzishika zake zake dhawabu,
  Daima na milele milele
Roho Ndiyo Itiayo Uzima
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYZaburi
REFJn 6:53 Ps 19
 • Comments