Salamu Ee Msalaba

Salamu Ee Msalaba
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Salamu Ee Msalaba Lyrics

Salamu, salamu, salamu, ee msalaba

 1. Salamu ee msalaba nakuabudu leo
  Ulalo wake Yesu kitanda cha uchungu
 2. Salamu ee msalaba, alama ya wokovu
  Shetani ukamshinda tufike uwinguni
 3. Salamu ee msalaba, lo Yesu atupenda
  Juu yako akalazwa kwa nia ya kuteswa
 4. Salamu, ee msalaba juu yako Mungu Mwana
  Awalipia watu, amwaga damu yake
 5. Salamu, ee msalaba, utupatie moyo
  Tuende njia njema, tufike uwinguni
 6. Salamu, ee msalaba, msalaba tupagae
  Tupande kilimani, mbinguni tutapona