Login | Register

Sauti za Kuimba

Sasa Ndio Wakati Lyrics

SASA NDIO WAKATI

 1. Sasa ndio wakati wa kutoa sadaka
  Kila mtu aanze kujifikiria

  Zilete zilete, zilete kwa Bwana
  Zilete zilete zilete kwa Bwana

 2. Tolea moyo wako, pia matendo yako
  Naye Bwana Mungu wangu, atakubariki
 3. Wiki nzima Bwana Mungu, amekulinda vyema
  Sasa nawe ndugu yangu, ujifikirie
 4. Kumbuka jinsi Yesu, alivyojitolea
  Pale msalabani, kwa ajili yako
 5. Baraka zake Mungu, za Baba na za Mwana
  Na za Roho Mtakatifu ziwe nanyi nyote
Sasa Ndio Wakati
CATEGORYOffertory/Sadaka
SOURCETanzania
 • Comments