Login | Register

Sauti za Kuimba

Michango Yenu Lyrics

MICHANGO YENU

@ J. C. Shomaly

{ Sasa ni wakati mwafaka wa kutoa sadaka yako ndugu
Hima ndugu jitolee kwa moyo wa ukarimu } *2
Iwe ni fedha pia hata mali umtolee Muumba wako
Akulindaye akuamshaye akupaye hewa na afya njema
{ Waumini, wote tuamke pamoja na sasa tujenge kanisa
Kanisa letu litasitawi kwa michango michango yetu } *2

 1. Kwa moyo wako wa ukarimu mpe muumba wako
  Sadaka yako kama shukrani yako
  Ujiulize kwa jinsi gani, Bwana kakubariki
  Umtolee kama shukrani yako.
 2. Wiki hii nzima amekulinda sasa jifikirie
  Ni kitu gani kiwe dhamana yako
  Umshukuru kwa jinsi gani naye afurahie
  Kwa mema mengi anayotenda kwangu,
 3. Wewe mzima ni wengi sana leo hawaamki
  Jifikirie ni wangapi umetenga
  Na familia yako daima shida haziwakumbi
  Si kwamba hao ni bora kuliko wote.
Michango Yenu
ALT TITLESasa ni Wakati Mwafaka
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMshike Mshike (Vol 5)
CATEGORYOffertory/Sadaka
 • Comments