Sasa Wakati Umefika

Sasa Wakati Umefika
ChoirSauti Tamu Melodies
AlbumZilipendwa
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerBasil Lukando
SourceTanzania
Skizaid sms to 811
VideoWatch on YouTube
Musical Notes
Timesignature2 2
MusickeyA Flat Major
NotesOpen PDF

Sasa Wakati Umefika Lyrics


Sasa wakati umefika, wa kushika nilicho nacho (mimi)
Kwa wema niende kwa Mungu nitoe zawadi
Sasa wakati umefika kwenda mbele ya Mungu wangu (mimi)
aone nilivyoandaa zawadi ya leo
Nitamwambia Bwana pokea hiki kidogo nilichonacho
Kwani Mungu wewe wanijua mimi siwezi hata kueleza
Nakusihi sana Baba unipokee
Nigawie na baraka niwe salama


1. Mema yote niliyokuwa nayo yametoka kwa Mungu
Hivyo nami ni kosa kusahau, kumshukuru
Kwani kuwepo hapa leo hii ni kazi ya nani
Kamwe mimi sitapata uwezo, pasipo Mungu

2. Mema aliyotenda Mungu nijibu lini na vipi,
Mbona hofu yazidi kuwa ndani, ya moyo wangu
Mbele ya Bwana Mungu wangu kufanya siri ni bure
Yeye ndiye mpanga mambo yote, ya wanadamu

3. Pumzi inayonipa uhai inatoka kwa nani
Bila Mungu hakika mwanadamu, siwezi kitu
Nimepata nafasi ya leo ya kwenda kutoa zawadi
Heri niende ya kesho sio yangu, ajua Mungu

4. Ewe mwumba wa vyote duniani na vyote mbinguni,
mimi leo nakuja kwako Baba, nihurumie.
Baba we ndiwe unayetawala kulala na kuamka kwangu,
Juu yangu utake nini Baba, kisifanyike.

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442