Sheria Ya Bwana Lyrics

SHERIA YA BWANA

@ Deo Mhumbira

{ Sheria ya Bwana, sheria ya Bwana ni kamilifu aee
Ni kamilifu aee huburudisha nafsi } *2

 1. Ushuhuda wa Bwana ushuhuda wa Bwana
  Ni amini ni amini humtia mjinga hekima
 2. Maagizo ya Bwana maagizo ya Bwana.
  Ni ya adili, ni ya adili huufurahisha moyo wangu
 3. Na amri yake Bwana amri yake Bwana,
  Ni safi sana, ni safi sana huyatia nuru macho yangu
 4. Hukumu zake Bwana hukumu zake Bwana
  Ni za kweli, ni za kweli nazo zina haki kabisa
Sheria Ya Bwana
COMPOSERDeo Mhumbira
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMNikiziangalia Mbingu (vol 18)
CATEGORYZaburi
REFPs. 19
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
8
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
NOTES Open PDF
 • Comments