Siku ya Kuja Lyrics

SIKU YA KUJA

 1. Siku yakuja kuuona mji wa Baba
  Wateule watafurahi waliookoka
  Siku ya kuja kuuona mji wa Baba,
  Tutaimba aleluya *2

  {Tutavikwa mavazi meupe yapendezayo sana} * 2
  {Wale waliookoka watavikwa kwa taji ya Bwana }
  {Sote tutaimba Mbinguni kwa furaha kubwa} * 2
  Alleluia Mungu wetu kwa upendo wako *2

 2. Tujitenge na mambo ya duniani
  Uongo, ulevi wizi visipatikane
  Ndipo tutakuwa washindi wake Bwana
  Tutaimba aleluya *2
Siku ya Kuja
CHOIR
CATEGORYGeneral
 • Comments