Login | Register

Sauti za Kuimba

Tazama Wazazi Lyrics

TAZAMA WAZAZI

@ J. C. Shomaly

 1. Tazama wazazi wazuri nilio nao
  Ni baba na mama walioyatenda haya
  Nidhamu na sala wamenifundisha kwa bidii
  Mapendo na wema wamenipa toka utotoni
  Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii
  Kwa zawadi hii ya wazazi alionipa

  Nikifikiria kiumbe wa Mungu mimi
  Nikifikiria ukuu wa Mungu kwangu
  Nikitafakari na matendo, anayotenda
  Kwa maisha yangu na wazazi, na ndugu zangu
  Ninashindwa kuyaelezea kwa kinywa changu
  Nitakaa kwake niyatafakari haya

 2. Tazama tazama elimu niliyo nayo
  Kumbuka wengine hakujaliwa hiyo
  Kwa nguvu ya neno na roho wake mtakatifu
  Kanipa nafasi ili nitumike kwa wengine
  Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii
  Kwa zawadi hii ya elimu aliyonipa
 3. Tazama tazama nchi hii nzuri nilimo
  Wengine za kwao hazina amani kamwe
  Amani furaha upendo na ukarimu huu
  uzuri wa watu wa mito milima na mabonde
  Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii
  Kwa zawadi hii ya nchi nilimozaliwa
Tazama Wazazi
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments