Tukuzeni Jina Lake Lyrics

TUKUZENI JINA LAKE

@ D. Wasonga

Tukuzeni Jina lake, milele na milele *2
Hubirini kwa watu ajabu zake zote
Semeni Bwana Mungu ni Bwana wa mabwana
{ Tangazeni kwa kuimba, kwa zaburi hata vinanda,
Na tarumbeta pia vinubi vyenye sauti ya kupendeza
Semeni ya kuwa ni Mfalme wa wafalme } *2

 1. Mpeni Bwana utukufu,
  Na nguvu pia mpeni, mwabuduni kwa uzuri wake,
  Kwa uzuri wa utakatifu, tetemekeeni mbele zake
 2. Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
  Mwimbieni Bwana wimbo mpya kwa maana ametenda
  Ametenda mambo ya ajabu machoni pa mataifa
 3. Paazeni sauti zenu,
  Mkiimba kwa furaha, kwa madaha ukirukaruka
  Ukicheza na kusimulia matendo yake ya ajabu
Tukuzeni Jina Lake
COMPOSERD. Wasonga
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CATEGORYZaburi
REFPs. 81
MUSIC KEYA Major
TIME SIGNATURE3
8
 • Comments