Tumsifu Mungu Lyrics

TUMSIFU MUNGU

@ Bernard Mukasa

TUMPENDE TUMSIFU MUNGU

 1. Tumpende tumsifu Mungu wetu wa milele na hata milele
  Tulisifu jina lake tukufu, na kulitangaza ulimwenguni

  {Tumsifu daima kwa heshima nyingi
  Ni Mungu kweli nasi tumsujudie } *2

 2. Duniani hapasimami, ni pahali pa kuiweka miguu yake
  Mbinguni ndipo aketipo , akiwaangalia wanadamu
 3. Azishikaye mbingu na mawingu, zikae imara zisidondoke
  Aupimaye mchana usizidi, wala usiku usididimike
 4. Ailindaye mimea ya jangwani, pasipo mvua wala maji mengi
  Azifanyaye bahari zidumu, hayo maji yake yasikauke
Tumsifu Mungu
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMungu Yule
CATEGORYZaburi
 • Comments