Tutaipataje Amani Lyrics

TUTAIPATAJE AMANI

@ J. C. Shomaly

Waumini na mataifa yote na jumuiya zo-te
Kama chemi chemi mo-ja, na tutafakarini pamoja } *2

Tutaipataje amani kwa bunduki nayo mabomu
Tutaipataje amani kwa migogoro ya siasa
Oooh inasikitisha, tumuombe Mungu atupe hekima
Oooh enyi mataifa, tumuombe Mungu atupe amani

 1. Mapanga hata marungu hayatasaidia, kupata amani
  Ugomvi kwa majirani hautasaidia, kupata amani
  Tuweke silaha chini tumuombe Mwenyezi, atupe hekima
  Tukae chini na wenzetu tujadiliane, tupate amani ae
 2. Makabila kupigana haitasaidia, kupata amani
  Mataifa kupigana haitasaidia, kupata amani
  Mzungu na Mwafrika sisi sote ni ndugu, tuombee amani
  Afrika na Ulaya sisi wana wa Mungu, tuombee amani ae
 3. Jumuiya mbalimbali tuungane pamoja, tuombee amani
  Afrika Mashariki nayo isiwe nyuma, tuombee amani
  Tanzania nayo Kenya sisi wana wa Mungu, tupendane sote
  Dunia yote sisi sote ni wana wa Mungu, tupendane sote ae
Tutaipataje Amani
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYTafakari
 • Comments