Uje Roho Mtakatifu Lyrics

UJE ROHO MTAKATIFU

@ Alfred Ossonga

Uje roho mtakatifu,
Uziendee nyoyo za waumini wako,
Uwatie mapendo yako, aleluya

 1. Roho ya Bwana imeujaza ulimwengu,
  Nayo itaviunganisha viumbe vyote
  Hujua maana ya kila sauti aleluya.
 2. Roho wa Bwana aliwafundisha watu wote
  Na wote wakatekwa na Roho Mtakatifu
  Wakisema matendo makuu ya Mungu aleluya
 3. Akawaunganisha watu wa lugha mbalimbali
  Wakaungana wote pamoja imani moja
  Watu wote wakamshangilia kwa furaha
 4. Tunakuomba uje ee Roho Mtakatifu
  Tufunulie siri za mbingu zilizofichwa
  Tujue ukweli wa rehema zako aleluya
Uje Roho Mtakatifu
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYRoho Mtakatifu (Pentecoste)
 • Comments