Umekosa Nini Yesu

Umekosa Nini Yesu
Alt TitleNjia ya Msalaba
Choir-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
SourceTraditional

Umekosa Nini Yesu Lyrics

 1. Tuifuate Njia ya Msalaba, tuifuate mpaka Kalvari
  Tusimamapo bila haya, (msalaba *2) huponya roho

  * * * * * *
 2. Umekosa Nini we Yesu, kushtakiwa bure kwa Pilato
  Wenye kustahili hukumu, si wewe, si wewe, Bwana ni sisi
 3. Ole msalaba huo mzito, apagazwa Mwana Mpenzi wa Mungu
  Mwili waenea mateso, alipa, alipa madhambi yetu
 4. Ona Mumba Mbingu na nchi, yupo chini mzigo wamwelemea
  Na mtu kiumbe chake kwa ukali, ampiga, ampiga bila huruma
 5. Huko njiani we Maria, waonaje hali ya mwanao
  Ni damu tupu na vidonda, machozi, machozi yamfumba macho
 6. Kwa Simoni heri ya kweli, mimi pia Yesu nisaidie
  Kuchukua mzigo wa ukombozi, kuteswa, kuteswa pamoja nawe
 7. Uso wa Yesu malaika, Bethlehemu wakuabudu
  Bahati yake Veronika, kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu
 8. Wakimvuta huku na huku, wauaji wakamchokesha bure
  Chini wamtupa bado kwa nguvu, aibu, aibu yao milele
 9. Wanawake wa Israeli, msilie kwa sababu hiyo
  Muwalilie hao kwa dhambi, upanga, upanga ni juu yao
 10. Mwokozi sasa ni ya tatu, kuanguka chini ya msalaba
  Katika dhambi za ulegevu, nijue, nijue kutubu hima
 11. Muje malaika wa Mbingu, funikeni mwiliwe kwa huruma
  Vidonda vyake na utupu, askari, askari wamvulia
 12. Hapo mkristu ushike moyo, Bwana wako alazwa msalabani
  Mara miguu na mikono, yafungwa, yafungwa kwa misumari
 13. Yesu mpenzi nakuabudu, msalabani unapohangaika
  Nchi yatetemeka kwa hofu, na jua, na jua linafifia
 14. Mama Maria mtakatifu, upokee maiti ya mwanao
  Tumemwua kwa dhambi zetu, twatubu, twatubu kwake na kwako
 15. Pamoja naye kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo
  Yesu tuwe wakristu wa kweli, twakupa, twakupa sasa mapendo

  * * * * * * * * *
 16. Katika roho yangu Bwana, chora mateso niliyokutesa
  Nisiyasahau madeni, na kazi, na kazi ya kuokoa