Login | Register

Sauti za Kuimba

Upokee Sadaka Yetu Lyrics

UPOKEE SADAKA YETU

 1. Upokee sadaka yetu *2,
  Ee Bwana Mungu – twakutolea
  Twakutolea – vipaji vyetu, Vipaji vyetu – sadaka kwako
 2. Upokee sadaka yetu *2,
  Ee Bwana Mungu –tunakuomba
  Tunakuomba – uzipokee, Uzipokee – sadaka zetu
 3. Upokee mazao yetu *2,
  Ee Bwana Mungu – ni mali yako
  Ni mali yako – twakutolea, Twakutolea – mazao yetu
 4. Upokee na fedha zetu *2,
  Ee Bwana Mungu –ni jasho letu
  Ni jasho letu – twakutolea, Twakutolea – ni jasho letu
 5. Upokee na shida zetu *2,
  Ee Bwana Mungu – tunakuomba
  Tunakuomba – uzipokee, Uzipokee – na shida zetu
 6. Upokee mkate wetu *2,
  Ee Bwana Mungu – ni kazi yetu
  Ni kazi yetu – tunayofanya, Tunayofanya – twakutolea
 7. Upokee divai yetu *2,
  Ee Bwana Mungu – ya mizabibu, Ya mizabibu –
  tunayopanda, Tunayopanda – kwa shamba zetu
Upokee Sadaka Yetu
CHOIR
CATEGORYOffertory/Sadaka
 • Comments